Overview
Semi is in bold:
Meaning in italics.
Examples in normal font, unformatted.
SEMI (IDIOMS)
- Kiguu na njia: Kutotulia mahali pamoja.
Ni vigumu sama kumpata Tanga ametulia nyumbani kwake. Yeye ni kiguu na njia.
- Lila na fila: Mema na mabaya.
Dunia huwa hivyo, harusi na matanga, lila na fila.
- Maji kuzidi unga: Mambo kuwa mabaya au kuharibika.
Maji ilipozidi unga ilibidi auze mali yake yote ili kuishi.
- Mate ya fisi: Tamaa kubwa.
Huyu mwanamume ana mate ya fisi, chochote anachokiona, anakitaka.
- Mdomo na pua: Kuwa karibu sana.
Najua anakoishi yule. Nyumbani kwangu na kwake ni mdomo na pua.
- Mkono wa birika: Kuwa mchoyo.
Jirani yule hata umuombe chumvi haezi kupa. Ana mkono wa birika.
- Shingo upande: Kufanya kitu bila kupenda.
Ingawa shingo upande, ilimbidi aiage familia yake ili aende kutafuta mapato.
- Uzi na sindano:
Ili kumaliza kujenga kanisa lile kwa muda wa mwezi moja, iliwabidi wanakijiji wafanye kazi kama uzi na sindano.
- Kuambulia patupu: Kukosa kabisa.
Jitihada zake za kumiliki mali ya mjomba wake ziliambulia patupu ilipojulikana kwamba aliyeaga alikuwa na mrithi dhahiri.
- Kuandaa meza: Kutayarisha chakula.
Mama alimuita Fatuma amusaidie kuandaa meza ili kuwapa wageni chakula.
- Kuasi ukapera:
Juma alivutiwa sana na Maria na hapo akajua kwamba msichana huyo pekee ndiye atamfanya kuasi ukapera.
- Kuchana mbuga: Kukimbia kutoka kwa hatari.
Wakazi walipomuona simba ameingia makaoni mwao walichana mbuga.
- Kuchomea nguru:
Wenye wivu hao walimuchomea nguru kwa bosi wake na kumsababisha asipandishwe cheo kazini.
- Kufa moyo: Kupoteza matumaini.
Yule mzazi alikufa moyo baada ya mtoto wake wa kipekee kuacha shule na kuanza kutumia dawa za kulevya.
- Kufua dafu: Kufaulu/Kushinda
Wakimbiaji kutika Kenya walifua dafu katika michezo ya Olimpiki.
- Kugonga mwamba:
Juhudi zake za kumuoa binti wa mfalme ziligonga mwamba.
- Kujifunga kibwebwe: Kutia bidii.
Rono alijifunga kibwewe katika mazoezi ili aweze kusajiliwa katika mashindano ya mbio.
- Kujikuna kichwa: Kufikiria sana.
Maswali ya mtihani hio yalinifanya nikune kichwa, yalikuwa magumu sana.
- Kukalia kuti kavu: Kutokuwa na mpango wa maisha ya baadaye.
Amekalia kuti kavu maana pesa zote alizopokea alitumia kwa raha na sasa ana madeni.
- Kukanyaga chechele: Kupotea njia.
Niliporudi kumtembelea Rehema nikiwa pekee yangu, nilikanyaga chechele.
- Kukosa mbele wala nyuma: Kuwa maskini sana.
Mwenye duka alimpa maskini yule mkate bila kumlipisha maana hana mbele wala nyuma.
- Kukata kamba: Kuaga dunia.
Mgonjwa yule aliyekuwa hospitalini muda wa mwaka moja amekata kamba.
- Kula kalenda: Kufungwa jela.
Anakula kalenda baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa uhalifu aliotenda.
- Kulaza damu: Kuwa mvivu.
Hakuna jambo linalo udhi kama kushiriki kazi na watu wanaopenda kulaza damu.
- Kumeza mate machungu: Kuvumilia dhiki.
Wafanyikazi wale wananyanyaswa na kazi hatari lakini wanameza mate chungu kwa sababu wanahitaji malipo.
- Kuwangukia miguuni: Kuomba msamaha.
Baada ya kuwatusi wazazi wake, aligundua makosa amefanya na kuwaangukia miguuni.
- Kung’oa nanga:
Meli ya kuelekea Ushelisheli iling’oa nanga mwendo wa saa mbili asubuhi.
- Kuona ashekari: Kupona.
Ali ameona ashekari baada ya kuugua malaria wiki lilopita.
- Kupandwa na mori:
Aliporudi nyumbani akamukosa mke wake na watoto alipandwa na mori.
- Kupiga darubini: Kufanya uchunguzi.
Mume yule alijipata matatani mke wake alipopiga darubini na kugundua kwamba anamutongoza mwanamke mwengine.
- Kupiga dua: Kuomba Mungu.
Shida zinapozidi, wao huenda kanisani kupiga dua.
- Kupiga hatua: Kuendelea mbele.
Alipiga hatua mara tu alipopata mtu wakudhamini mradi wake.
- Kupiga miayo: Kupanua kinywa na kutoa pumzi kama dalili ya usingizi, njaa au kuchoka.
Mwalimu alipoendelea kufunza baada ya kengele ya chakula cha mchana kupigwa, wanafunzi walianza kupiga miayo.
- Kupiga moyo konde: Kujipa nguvu.
Mhubiri aliwahimiza kupiga moyo konde wakati wanapokabiliwa na mateso za kidunia.
- Kupigwa kalamu: Kufutwa kazi.
Baba yake alikosa pesa za kumlipia ada katika chuo kikuu baada ya kupigwa kalamu.
- Kushukiwa na nyota ya jaha: Kuwa na bahati.
Kila anapocheza mchezo wa bahati nasibu, yeye hushukiwa na nyota ya jaha maana hakosi kushinda.
- Kutafuta unga: Kufanya kazi.
Kazi ni kazi, mtu hachagui, lazima kutafuta unga.
- Kutoa mkono wa tanzia: Kumpa mtu pole wakati wa msiba.
Mfanyakazi mwenzetu alipofiwa na mwenziwe, tulienda kumtembelea ili kumpa mkono wa tanzia.
- Kutiwa mbaroni:
Ukivunja sheria utatiwa mbaroni.
- Kutoa lulu: Kuongea maneno yaliyo na busara.
Kila anapozungumza, raia wote humsikiza maana ye hutoa lulu.
- Kutoa ngebe: Kuongea maneno mengi yasiyo na maana.
Mwanasiasa yule hana muhimu la kutueleza. Kazi yake ni kutoa ngebe.
- Kutonesha kidonda: Kumbusha kitu kinachoumiza.
Halima hana furaha. Mpenzi wake wa sasa amerudia makosa ya mpenzi wake wa kale. Amemtonesha kidonda.
- Kutumbukia kisimani: Kuingia katika shida ambayo ni ngumu kujitoa.
Mtalii alipokamatwa bila pasipoti au cheti chochote cha kujitambulisha, alijua ametumbukia kisimani.
- Kutupa macho: Kuangalia mbali unapotafuta kitu.
Ndege ilipotua, alitupa macho katika umati wa watu akimtafuta mgeni wake.
- Kuvalia miwani:
Daktari alimuonya kwamba aache kunywa pombe lakini akaivalia miwani onyo hilo.
- Kuvuliwa mbeleko:
Amina alivuliwa mbeleko baada ya rafikiye kutangaza mambo yake ya siri hadharani.
- Kuvunja ungo: Kukomaa kwa mtoto wa kike.
Sanasana wasichana huvunga ungo wakifikisha miaka kumi na tatu.
- Kuzunguka mbuyu: Kutoa hongo/rushwa.
Yule polisi alimtaka dereva azunguke mbuyu ndiposa aliwachilie gari lake.
- Kwenda mrama: Kuharibikia kwa jambo au mambo.
Maisha ilipomwendea mrama, aliamua kujiua.
- Kwenda msalani: Kwenda chooni.
Mwanafunzi aliposhindwa na mazoezi ya ziada, alimuomba mwalimu ruhusa ya kwenda msalani.