Overview
Methali is in bold:
Meaning in italics.
Examples in normal font, unformatted.
METHALI(PROVERBS)
- Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo: Binadamu muungwana hutambulika na matendo yake wala si maneno asemayo, mavazi wala maumbile.
Waeza nena unavyotaka ili upewe kazi ile lakini jua kwamba ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo.
- Akili ni mali: Kuwa na akili husaidia mtu kuwa na maarifa ya kutengeneza mali.
Nenda shule usome na kuongeza maarifa kwani baadaye itakusaidia. Akili ni mali.
- Akili ni nywele, kila mtu ana zake: Akili ni za aina nyingi na za kipekee kwa kila binadamu.
Yule kocha wa zamani alitumia mkakati mwingine, na huyu mgeni ametumia tofauti lakini bado timu yetu ilifuzi. Kwa kweli, akili ni ywele kila mtu ana zake.
- Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu: Mtoto asiyeadhibiwa nyumbani na mzazi atahangaika baadaye duniani.
Kijana yule maisha imemuendea mrama. Amepigwa kalamu kazini kwa sababu ya ulevi na utundu na pia hajui kutafuta kazi ingine. Asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
- Asiyekubali kushindwa, si mshindani: Mshindani kamili hukubali matokeo bila chuki wala uchungu.
Sipendi kucheza mpira na Yuanita. Nikimshinda yeye hukasirika na kubishana na asiyekubali kushindwa si mshindani.
- Baada ya dhiki faraja: Amani na faraja huja baada ya muda wa shida na matatizo.
Najua unapitia mengi machungu kwa sasa lakini jipe moyo. Kumbuka baada ya dhiki faraja.
- Bandubandu humaliza gogo: Juhudi ndogo ndogo humaliza changamoto kubwa.
Bosi amenipa kazi nyingi sijui naanzia wapi. Anza kidogo kidogo utamaliza, bandubandu humaliza gogo.
- Chanda chema huvishwa pete: Jambo jema husifiwa na kutuzwa.
Kazi yake mzuri ilimuezesha kutuzwa kama mfano bora kwa jamii. Kwa kweli, chanda chema huvishwa pete.
- Chema chajiuza, kibaya chajitembeza: Kitu kizuri hakiitaji kupigiwa debe kwani kitajiuza chenyewe, bali kibaya lazima kijitangaze.
Mimi hupendelea vifaa vya elektroniki kutako Ujerumani au Japan. Hizi zingine zapitishwa hapa kila siku ni bandia. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
- Dalili ya mvua ni mawingu: Kama vile mawingu meusi huonekana kabla ya mvua, ndivyo dalili ya mambo hutokea kabla yafanyike.
Msimamizi wako kazini amechukua kibali chako na kukuhakiki vibaya mwezi uliopita na bado unarejea kazini? Dalili ya mvua ni mawingu, anza kutafuta kazi ingine.
- Damu ni nzito kuliko maji: Watu wa ukoo moja huwa pamoja kwa nguvu ukilinganisha na jamaa wa mbali.
Kwa chochote unachofanya au popopte unaenda, usiisahau jamii yako. Kumbuka kwamba damu ni nzito kuliko maji.
- Dawa ya moto ni moto: Jambo ambalo limesemwa au kutendwa hulipizwa na lingine kama hilo.
Alimtusi mwenzake na kumfanya ahisi vibaya naye pia ametusiwa hivyohivyo na anasikia vibaya. Kweli dawa ya moto ni moto.
- Dua la kuku halimpati mwewe: Kilio cha mnyonge hakiwezi kumhangaisha mtesi wake au aliye na nguvu kumshinda.
Maskwota waliomba serikali na waliomiliki ardhi wawape muda watafuta makao mengine kabla ya kuwatimua, lakini wapi. Kwa kweli, dua la kuku halimpati mwewe.
- Fadhila ya punda ni mateke: Kuna watu ambao ukishawasaidia wanakuumiza.
Baada ya kumpa akiba yangu ili aanze biashara ya kumsaidia, aliniibia mali yangu yote na kunifungia mlango, kweli fadhila ya punda ni mateke.
- Fimbo ya mbali haiuwi nyoka: Unapopata shida, ni watu walio karibu nawe ndio wanaweza kukusaidia bali wa mbali hawatajua kinachoendelea.
Usiwe mgumu kwa majirani wako, waeza pata shida wakati mmoja na fimbo ya mbali haiuwi nyoka.
- Fuata nyuki ule asali: Ukitaka kufaulu maishani, jihusishe na watu ambao wamefaulu.
Napendelea kuwatembelea akina Tanasha maana kwao kuna mazuri. Nafwata nyuki nile asali.
- Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno: Kitu ambacho hakina maana kwa aliye naye, ni cha muhimu sana kwa aliye kosa.
Usichome nguo zako ambazo zimekua matambara zitamsaidia mwengine. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.
- Haba na haba hujaza kibaba: Mazao makubwa huanza na madogo.
Nilianza hii biashara na akiba ambapo nilikuwa naeka kando shilingi hamsini kila wiki. Sasa natambua kwamba haba na haba hujaza kibaba.
- Haraka haraka haina baraka: Mambo ambayo kufanywa haraka bila kutilia maanani huwa hayafuzu.
Enda polepole, umemjua msichana yule tu juzi na sasa wataka kumuoa? Haraka haraka haina baraka ndugu.
- Hasira hasara: Kawaida, binadamu aishikwa na hasira hufanya vitendo ambavyo vitamgharimu.
Wanafunzi walichoma shule kwa hasira ya kupewa mtihani ngumu. Sasa ni wao wameambiwa wagharamie ujenzi upya wa shule hio. Hasira hasara.
- Heri kujikwa kidole kuliko ulimi: Afadhali kujigonga na kujiumiza kidole, badala ya kusema maneno ambayo hukutarajia kusema.
Sijui kama Anita atanisamehe baada ya kuropokwa siri yake kwa mamake. Heri ningejikwa kidole kuliko ulimi.
- Jino la pembe si dawa ya pengo: Kitu ambacho huekwa kushikilia nafasi ya kile hakiko, huwa haiwi kitu hicho.
Waeza badili ngozi lako na kemikali uwe mweupe ka mwangaza lakini uzazi wako bado utafwata ngozi nyeusi. Kumbuka kwamba jino la pembe si dawa ya pengo.
- Jogoo la shamba haliwiki mjini: Mtu anaeza kuwa na ushawishi mkubwa mahali fulani lakini pengine hapana.
Yule mkuu wa kijiji alipeleka kanuni zake nchi mgeni alipoenda kuzuru. Hakuna aliyemsikiza na hapo akajua kwamba jogoo la shamba haliwiki mjini.
- Kenda karibu ya kumi: Usife moyo unapofanya jambo kwa sababu unakaribia kufaulu.
Fanya marudio yote ya mazoezi ndo upate uzito ungependa kwani kenda karibu ya kumi.
- Kidole kimoja hakivunji chawa: Ni bora kushirikiana kwa sababu mtu mmoja pekee yake hawezi kutenda makubwa.
Itabidi tusaidiane kujengea watoto wetu shule kwani kidole kimoja hakivunji chawa.
- Kitanda usichokilala hujui kunguni wake: Huwezi elewa shida ambazo hujazipitia.
Usimwambie mtu aliye na huzuni agutuke na kufurahi ka wewe mwenyewe hujapitia huzuni hio. Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
- Kucha Mungu si kilemba cheupe: Kuvaa au kuonekana kwa mtu jinsi dini inaagiza si hakikisho ya uaminifu wake.
Wafuasi hawa hupita hapa kila asubuhi wamevaa mavazi meupe na kuweka mikono yao pamoja kwa sala lakini wamesahau kwamba kucha Mungu si kilemba cheupe.
- Kuishi kwingi kuona mengi: Wazee, au watu ambao wana miaka mingi duniani wana maarifa ya mambo mengi.
Mimi kama babu yako ninakushauri usimuoe msichana kutoka lile boma. Utakuja kuhangaika. Ninajua kwa sababu, kuishi kwingi, kuona mengi.
- Kukopa harusi kulipa matanga: Kuna watu ambao huomba kwa urahisi sana lakini kurudisha kile walichoomba inakuwa shida.
Huyi alinililia hapa nimukopeshe elfu kumi atarudisha mwisho wa mwezi. Sasa yaelekea miezi tatu nikimuitisha pesa zangu ananipa udhuru baada ya ingine. Kweli, kukopa ni harusi kulipa matanga.
- Kupotea ndiyo kujua njia: Mtu anapokosa kufaulu, yeye hugundua namna ya kufaulu kutokana na funzo hilo.
Usioena aibu kwa kutofaulu kwa kazi ulioifanya, saa zingine kupotea ndiyo kujua njia.
- La kuvunda halina ubani: Hakuna kitu ambacho kinaeza funika matokeo ya kitu ambacho kishaharibika.
Polisi walipofika kusaka nyumba ya mteka nyara, alijaribu kuficha vitendo vyake lakini zikajitokeza wazi; la kuvunda halina ubani.
- Maji yaliyomwagika hayazoleki: Jambo likiharibika huwa limeharibika hata litengenezwe aje, halitakuwa kama awali.
Nilitaka tuanze familia baada ya miaka mbili ya ndoa lakini tayari mke wangu ameshika mimba. Itabidi nikubali tu kwa sababu maji yaliyomwagika hayazoleki.
- Milima haikutani, lakini binadamu hukutana: Ukimuaga mtu kwaheri kuna matumaini kwamba mtakutana baadaye tena. Pia ukimtendea mtu maovu jua mtakutana baadaye labda ikiwa ni wewe uko na shida na wahitaji msaada wake.
Naenda ng’ambo masomoni na wewe unaenda kuzuru dunia. Natumai kwamba siku moja tutapatana tena. Milima haikutani, binadamu hukutana.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo: Kuwaonya wazazi wasiogope kuwaadhibu watoto wao kama wanataka wakuwe wangwana maishani.
Mama yule amemdekeza mwana wake hadi amefika miaka thelathini na hajui inafaa atoke nyumbani aanze kujitegemea. Kwe kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Mtoto wa nyoka ni nyoka: Mara nyingi mtoto hufanana na kuchukua tabia za mzazi wake.
Kijana huyu anawafukuza mabinti mtaani kama vile babake alifanya akiwa umri wake. Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka.
- Ndovu wawili wakipigana nyasi huumia: Walio na nguvu wakizozana, wadhaifu ndio huumia.
Wanasiasa wakenya wakikosa kusikilizana, raia wakawaida ndio huteseka, kwani, ndovu wawili wakipigana, nyasi huumia.
- Paka akiondoka panya hutawala: Mkubwa akiondoka, wadogo wake hufanya mambo jinsi watakavyo.
Watoto hao walingoja wazazi wao wondoke kisha walete rika zao nyumbani kwa sherehe; enyewe, paka akiondoka, panya utawala.
- Panapofuka moshi hapakosi moto: Ka vile moshi huashiria moto, ukiona watu wanatetana juu ya jambo linakaa ndogo kuna lingine kubwa nyuma yake.
Niliona jinsi alimwangalia na ukali nikajua hapa kuna jambo. Panapofuka moshi hapakosi moto.
- Penye nia ipo njia: Mtu anapokuwa na dhamira ya kutenda jambo kutoka kwa dhati, haezi kosa njia ya kuitekeleza.
Kijiji hiki hakina bwawa la maji lakini tutajitahidi na kutengeneza moja hivi karibuni. Penye nia hapakosi njia.
- Pilipili usozila zakuwashiani?: Mambo yasiyokuhusu mbona yakutatize?
Mbona ulienda kumpa Salim msomo kuhusu mke wake? Pilipili usozila zakuwashiani?
- Samaki moja akioza huoza wote: Ukijihusisha na watu wanaotenda mambo mabaya ni rahisi kwako pia kuanza kutenda kama hao.
Kijana yule anapenda sana kuranda na hii gengi ya kuuza dawa za kulevya. Sidhani ni mzuri maana samaki moja akioza huoza wote.
- Sikio halilali njaa: Siku haiezi pita bila mtu kukosa kusikiza neno.
Bila kuulizia, niliambiwa kwamba Kamau ana mpango wa kumtalaki mke wake. Sikio halilali njaa.
- Siku njema huonekana asubuhi: Kama matokeo ya jambo yatakuwa mema, dalili huanza kuonekana mapema.
Siwezi amua leo maana nilianza siku na visirani mingi sana, na ujuavyo siku njema huonekana asubuhi.
- Siku za mwizi ni arobaini: Endelea kufanya maovu lakini siku yako ya hukumu itafika.
Amezoea kuingia kwa shamba ya jirani yake wakati hayupo ili kuiba matunda. Leo amepatikana bila kutarajia. Kwa kweli siku za mwizi ni arobaini.
- Tabia ni ngozi: Ni vigumu kwa mtu kubadili tabia maana imeshikana na mwili wake kama ngozi.
Aliniahidi ataacha kunywa pombe nikikubali kuolewa naye lakini wapi, tabia ni ngozi.
- Tamaa mbele mauti nyuma: Anayetanguliza tamaa na ubinafsi huwa na mwisho mbaya.
Mvulana yule alijiunga na jambazi ili kujitajirisha haraka na sasa polisi wamempiga risasi. Angejua tamaa mbele mauti nyuma.
- Ukiona vinaelea, jua vimeundwa: Ukiona kitu kinakaa kizuri na kinafanya kazi yake inavyotakikana jua kwamba ni bidii na maarifa ya mtu mwingine imetoa matokeo hayo.
Jana nilitembelea kiwanda cha kutengeneza gari na macho yangu yalifurahihswa kweli. Ukiona vyaelea kweli, jua vimeundwa.
- Usipoziba ufa utajenga ukuta: Usiporekebisha tatizo kama lingali changa utagharamia pakubwa baadaye.
Mtoto huyu ameanza utundu. Hebu muonye mapema maana usipoziba ufa utajenga ukuta.
- Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo: Mambo yaliyopita tuachana nayo hayatudhuru, tuwaze tutavyokabiliano na yanayoukuja.
Mbona unaturudisha nyuma na kuna shida kubwa zaidi yaja? Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
- Yote yang’aayo si dhahabu: Usipende kitu kwa uzuri wake wa nje kwa maana si kila kitu kinachomeremeta kwa nje ni nzuri kwa ndani.
Jana nikiwa pwani nilimuona binti mrembo yuavutia sana. Karibu niende kumlaki lakini nikakumbuka babu alinionya, yote yang’aayo si dhahabu.