{"id":2236,"date":"2019-08-20T14:49:11","date_gmt":"2019-08-20T14:49:11","guid":{"rendered":"http:\/\/theskrypt.co.ke\/?page_id=2236"},"modified":"2019-11-19T17:53:35","modified_gmt":"2019-11-19T17:53:35","slug":"learn-kiswahili","status":"publish","type":"page","link":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/kiswahili\/learn-kiswahili\/","title":{"rendered":"Proverbs"},"content":{"rendered":"<h2><u>Overview<\/u><\/h2>\n<p><strong>Methali is in bold:<\/strong><\/p>\n<p><em>Meaning in italics.<\/em><\/p>\n<p>Examples in normal font, unformatted.<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<h3><strong>METHALI(PROVERBS)<\/strong><\/h3>\n<ol>\n<li><strong>Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo:<\/strong> <em>Binadamu muungwana hutambulika na matendo yake wala si maneno asemayo, mavazi wala maumbile<\/em>.<\/li>\n<\/ol>\n<p>Waeza nena unavyotaka ili upewe kazi ile lakini jua kwamba ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo.<\/p>\n<ol start=\"2\">\n<li><strong>Akili ni mali:<\/strong> <em>Kuwa na akili husaidia mtu kuwa na maarifa ya kutengeneza mali.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Nenda shule usome na kuongeza maarifa kwani baadaye itakusaidia. Akili ni mali.<\/p>\n<ol start=\"3\">\n<li><strong>Akili ni nywele, kila mtu ana zake: <\/strong><em>Akili ni za aina nyingi na za kipekee kwa kila binadamu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Yule kocha wa zamani alitumia mkakati mwingine, na huyu mgeni ametumia tofauti lakini bado timu yetu ilifuzi. Kwa kweli, akili ni ywele kila mtu ana zake.<\/p>\n<ol start=\"4\">\n<li><strong>Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu<\/strong>: <em>Mtoto asiyeadhibiwa nyumbani na mzazi atahangaika baadaye duniani.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kijana yule maisha imemuendea mrama. Amepigwa kalamu kazini kwa sababu ya ulevi na utundu na pia hajui kutafuta kazi ingine. Asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.<\/p>\n<ol start=\"5\">\n<li><strong>Asiyekubali kushindwa, si mshindani:<\/strong> <em>Mshindani kamili hukubali matokeo bila chuki wala uchungu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Sipendi kucheza mpira na Yuanita. Nikimshinda yeye hukasirika na kubishana na asiyekubali kushindwa si mshindani.<\/p>\n<ol start=\"6\">\n<li><strong>Baada ya dhiki faraja:<\/strong> <em>Amani na faraja huja baada ya muda wa shida na matatizo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Najua unapitia mengi machungu kwa sasa lakini jipe moyo. Kumbuka baada ya dhiki faraja.<\/p>\n<ol start=\"7\">\n<li><strong>Bandubandu humaliza gogo:<\/strong> <em>Juhudi ndogo ndogo humaliza changamoto kubwa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Bosi amenipa kazi nyingi sijui naanzia wapi. Anza kidogo kidogo utamaliza, bandubandu humaliza gogo.<\/p>\n<ol start=\"8\">\n<li><strong>Chanda chema huvishwa pete:<\/strong> <em>Jambo jema husifiwa na kutuzwa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kazi yake mzuri ilimuezesha kutuzwa kama mfano bora kwa jamii. Kwa kweli, chanda chema huvishwa pete.<\/p>\n<ol start=\"9\">\n<li><strong>Chema chajiuza, kibaya chajitembeza:<\/strong> <em>Kitu kizuri hakiitaji kupigiwa debe kwani kitajiuza chenyewe, bali kibaya lazima kijitangaze.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mimi hupendelea vifaa vya elektroniki kutako Ujerumani au Japan. Hizi zingine zapitishwa hapa kila siku ni bandia. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.<\/p>\n<ol start=\"10\">\n<li><strong>Dalili ya mvua ni mawingu<\/strong>: <em>Kama vile mawingu meusi huonekana kabla ya mvua, ndivyo dalili ya mambo hutokea kabla yafanyike.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Msimamizi wako kazini amechukua kibali chako na kukuhakiki vibaya mwezi uliopita na bado unarejea kazini?\u00a0 Dalili ya mvua ni mawingu, anza kutafuta kazi ingine.<\/p>\n<ol start=\"11\">\n<li><strong>Damu ni nzito kuliko maji:<\/strong> <em>Watu wa ukoo moja huwa pamoja kwa nguvu ukilinganisha na jamaa wa mbali.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kwa chochote unachofanya au popopte unaenda, usiisahau jamii yako. Kumbuka kwamba damu ni nzito kuliko maji.<\/p>\n<ol start=\"12\">\n<li><strong>Dawa ya moto ni moto: <\/strong><em>Jambo ambalo limesemwa au kutendwa hulipizwa na lingine kama hilo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Alimtusi mwenzake na kumfanya ahisi vibaya naye pia ametusiwa hivyohivyo na anasikia vibaya. Kweli dawa ya moto ni moto.<\/p>\n<ol start=\"13\">\n<li><strong>Dua la kuku halimpati mwewe: <\/strong><em>Kilio cha mnyonge hakiwezi kumhangaisha mtesi wake au aliye na nguvu kumshinda.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Maskwota waliomba serikali na waliomiliki ardhi wawape muda watafuta makao mengine kabla ya kuwatimua, lakini wapi. Kwa kweli, dua la kuku halimpati mwewe.<\/p>\n<ol start=\"14\">\n<li><strong>Fadhila ya punda ni mateke:<\/strong> <em>Kuna watu ambao ukishawasaidia wanakuumiza.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Baada ya kumpa akiba yangu ili aanze biashara ya kumsaidia, aliniibia mali yangu yote na kunifungia mlango, kweli fadhila ya punda ni mateke.<\/p>\n<ol start=\"15\">\n<li><strong>Fimbo ya mbali haiuwi nyoka:<\/strong> <em>Unapopata shida, ni watu walio karibu nawe ndio wanaweza kukusaidia bali wa mbali hawatajua kinachoendelea.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Usiwe mgumu kwa majirani wako, waeza pata shida wakati mmoja na fimbo ya mbali haiuwi nyoka.<\/p>\n<ol start=\"16\">\n<li><strong>Fuata nyuki ule asali<\/strong>: <em>Ukitaka kufaulu maishani, jihusishe na watu ambao wamefaulu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Napendelea kuwatembelea akina Tanasha maana kwao kuna mazuri. Nafwata nyuki nile asali.<\/p>\n<ol start=\"17\">\n<li><strong>Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno<\/strong>: <em>Kitu ambacho hakina maana kwa aliye naye, ni cha muhimu sana kwa aliye kosa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Usichome nguo zako ambazo zimekua matambara zitamsaidia mwengine. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.<\/p>\n<ol start=\"18\">\n<li><strong>Haba na haba hujaza kibaba:<\/strong> <em>Mazao makubwa huanza na madogo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Nilianza hii biashara na akiba ambapo nilikuwa naeka kando shilingi hamsini kila wiki. Sasa natambua kwamba haba na haba hujaza kibaba.<\/p>\n<ol start=\"19\">\n<li><strong>Haraka haraka haina baraka:<\/strong> <em>Mambo ambayo kufanywa haraka bila kutilia maanani huwa hayafuzu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Enda polepole, umemjua msichana yule tu juzi na sasa wataka kumuoa? Haraka haraka haina baraka ndugu.<\/p>\n<ol start=\"20\">\n<li><strong>Hasira hasara: <\/strong><em>Kawaida, binadamu aishikwa na hasira hufanya vitendo ambavyo vitamgharimu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Wanafunzi walichoma shule kwa hasira ya kupewa mtihani ngumu. Sasa ni wao wameambiwa wagharamie ujenzi upya wa shule hio. Hasira hasara.<\/p>\n<ol start=\"21\">\n<li><strong>Heri kujikwa kidole kuliko ulimi:<\/strong> <em>Afadhali kujigonga na kujiumiza kidole, badala ya kusema maneno ambayo hukutarajia kusema.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Sijui kama Anita atanisamehe baada ya kuropokwa siri yake kwa mamake. Heri ningejikwa kidole kuliko ulimi.<\/p>\n<ol start=\"22\">\n<li><strong>Jino la pembe si dawa ya pengo:<\/strong> <em>Kitu ambacho huekwa kushikilia nafasi ya kile hakiko, huwa haiwi kitu hicho.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Waeza badili ngozi lako na kemikali uwe mweupe ka mwangaza lakini uzazi wako bado utafwata ngozi nyeusi. Kumbuka kwamba jino la pembe si dawa ya pengo.<\/p>\n<ol start=\"23\">\n<li><strong>Jogoo la shamba haliwiki mjini:<\/strong> <em>Mtu anaeza kuwa na ushawishi mkubwa mahali fulani lakini pengine hapana.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Yule mkuu wa kijiji alipeleka kanuni zake nchi mgeni alipoenda kuzuru. Hakuna aliyemsikiza na hapo akajua kwamba jogoo la shamba haliwiki mjini.<\/p>\n<ol start=\"24\">\n<li><strong>Kenda karibu ya kumi<\/strong>: <em>Usife moyo unapofanya jambo kwa sababu unakaribia kufaulu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Fanya marudio yote ya mazoezi ndo upate uzito ungependa kwani kenda karibu ya kumi.<\/p>\n<ol start=\"25\">\n<li><strong>Kidole kimoja hakivunji chawa: <\/strong><em>Ni bora kushirikiana kwa sababu mtu mmoja pekee yake hawezi kutenda makubwa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Itabidi tusaidiane kujengea watoto wetu shule kwani kidole kimoja hakivunji chawa.<\/p>\n<ol start=\"26\">\n<li><strong>Kitanda usichokilala hujui kunguni wake: <\/strong><em>Huwezi elewa shida ambazo hujazipitia.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Usimwambie mtu aliye na huzuni agutuke na kufurahi ka wewe mwenyewe hujapitia huzuni hio. Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.<\/p>\n<ol start=\"27\">\n<li><strong>Kucha Mungu si kilemba cheupe<\/strong>: <em>Kuvaa au kuonekana kwa mtu jinsi dini inaagiza si hakikisho ya uaminifu wake.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Wafuasi hawa hupita hapa kila asubuhi wamevaa mavazi meupe na kuweka mikono yao pamoja kwa sala lakini wamesahau kwamba kucha Mungu si kilemba cheupe.<\/p>\n<ol start=\"28\">\n<li><strong>Kuishi kwingi kuona mengi: <\/strong><em>Wazee, au watu ambao wana miaka mingi duniani wana maarifa ya mambo mengi.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mimi kama babu yako ninakushauri usimuoe msichana kutoka lile boma. Utakuja kuhangaika. Ninajua kwa sababu, kuishi kwingi, kuona mengi.<\/p>\n<ol start=\"29\">\n<li><strong>Kukopa harusi kulipa matanga:<\/strong> <em>Kuna watu ambao huomba kwa urahisi sana lakini kurudisha kile walichoomba inakuwa shida.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Huyi alinililia hapa nimukopeshe elfu kumi atarudisha mwisho wa mwezi. Sasa yaelekea miezi tatu nikimuitisha pesa zangu ananipa udhuru baada ya ingine. Kweli, kukopa ni harusi kulipa matanga.<\/p>\n<ol start=\"30\">\n<li><strong>Kupotea ndiyo kujua njia:<\/strong> <em>Mtu anapokosa kufaulu, yeye hugundua namna ya kufaulu kutokana na funzo hilo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Usioena aibu kwa kutofaulu kwa kazi ulioifanya, saa zingine kupotea ndiyo kujua njia.<\/p>\n<ol start=\"31\">\n<li><strong>La kuvunda halina ubani:<\/strong> <em>Hakuna kitu ambacho kinaeza funika matokeo ya kitu ambacho kishaharibika.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Polisi walipofika kusaka nyumba ya mteka nyara, alijaribu kuficha vitendo vyake lakini zikajitokeza wazi; la kuvunda halina ubani.<\/p>\n<ol start=\"32\">\n<li><strong>Maji yaliyomwagika hayazoleki: <\/strong><em>Jambo likiharibika huwa limeharibika hata litengenezwe aje, halitakuwa kama awali.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Nilitaka tuanze familia baada ya miaka mbili ya ndoa lakini tayari mke wangu ameshika mimba. Itabidi nikubali tu kwa sababu maji yaliyomwagika hayazoleki.<\/p>\n<ol start=\"33\">\n<li><strong>Milima haikutani, lakini binadamu hukutana:<\/strong> <em>Ukimuaga mtu kwaheri kuna matumaini kwamba mtakutana baadaye tena. Pia ukimtendea mtu maovu jua mtakutana baadaye labda ikiwa ni wewe uko na shida na wahitaji msaada wake.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Naenda ng\u2019ambo masomoni na wewe unaenda kuzuru dunia. Natumai kwamba siku moja tutapatana tena. Milima haikutani, binadamu hukutana.<\/p>\n<ol start=\"34\">\n<li><strong>Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo:<\/strong> <em>Kuwaonya wazazi wasiogope kuwaadhibu watoto wao kama wanataka wakuwe wangwana maishani.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mama yule amemdekeza mwana wake hadi amefika miaka thelathini na hajui inafaa atoke nyumbani aanze kujitegemea. Kwe kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.<\/p>\n<ol start=\"35\">\n<li><strong>Mtoto wa nyoka ni nyoka: <\/strong><em>Mara nyingi mtoto hufanana na kuchukua tabia za mzazi wake.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kijana huyu anawafukuza mabinti mtaani kama vile babake alifanya akiwa umri wake. Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka.<\/p>\n<ol start=\"36\">\n<li><strong>Ndovu wawili wakipigana nyasi huumia: <\/strong><em>Walio na nguvu wakizozana, wadhaifu ndio huumia.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Wanasiasa wakenya wakikosa kusikilizana, raia wakawaida ndio huteseka, kwani, ndovu wawili wakipigana, nyasi huumia.<\/p>\n<ol start=\"37\">\n<li><strong>Paka akiondoka panya hutawala: <\/strong><em>Mkubwa akiondoka, wadogo wake hufanya mambo jinsi watakavyo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Watoto hao walingoja wazazi wao wondoke kisha walete rika zao nyumbani kwa sherehe; enyewe, paka akiondoka, panya utawala.<\/p>\n<ol start=\"38\">\n<li><strong>Panapofuka moshi hapakosi moto:<\/strong> <em>Ka vile moshi huashiria moto, ukiona watu wanatetana juu ya jambo linakaa ndogo kuna lingine kubwa nyuma yake.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Niliona jinsi alimwangalia na ukali nikajua hapa kuna jambo. Panapofuka moshi hapakosi moto.<\/p>\n<ol start=\"39\">\n<li><strong>Penye nia ipo njia:<\/strong> <em>Mtu anapokuwa na dhamira ya kutenda jambo kutoka kwa dhati, haezi kosa njia ya kuitekeleza.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kijiji hiki hakina bwawa la maji lakini tutajitahidi na kutengeneza moja hivi karibuni. Penye nia hapakosi njia.<\/p>\n<ol start=\"40\">\n<li><strong>Pilipili usozila zakuwashiani?:<\/strong> <em>Mambo yasiyokuhusu mbona yakutatize?<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mbona ulienda kumpa Salim msomo kuhusu mke wake? Pilipili usozila zakuwashiani?<\/p>\n<ol start=\"41\">\n<li><strong>Samaki moja akioza huoza wote: <\/strong><em>Ukijihusisha na watu wanaotenda mambo mabaya ni rahisi kwako pia kuanza kutenda kama hao.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kijana yule anapenda sana kuranda na hii gengi ya kuuza dawa za kulevya. Sidhani ni mzuri maana samaki moja akioza huoza wote.<\/p>\n<ol start=\"42\">\n<li><strong>Sikio halilali njaa: <\/strong><em>Siku haiezi pita bila mtu kukosa kusikiza neno<\/em>.<\/li>\n<\/ol>\n<p>Bila kuulizia, niliambiwa kwamba Kamau ana mpango wa kumtalaki mke wake. Sikio halilali njaa.<\/p>\n<ol start=\"43\">\n<li><strong>Siku njema huonekana asubuhi:<\/strong> <em>Kama matokeo ya jambo yatakuwa mema, dalili huanza kuonekana mapema.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Siwezi amua leo maana nilianza siku na visirani mingi sana, na ujuavyo siku njema huonekana asubuhi.<\/p>\n<ol start=\"44\">\n<li><strong>Siku za mwizi ni arobaini<\/strong>: <em>Endelea kufanya maovu lakini siku yako ya hukumu itafika.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Amezoea kuingia kwa shamba ya jirani yake wakati hayupo ili kuiba matunda. Leo amepatikana bila kutarajia. Kwa kweli siku za mwizi ni arobaini.<\/p>\n<ol start=\"45\">\n<li><strong>Tabia ni ngozi: <\/strong><em>Ni vigumu kwa mtu kubadili tabia maana imeshikana na mwili wake kama ngozi.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Aliniahidi ataacha kunywa pombe nikikubali kuolewa naye lakini wapi, tabia ni ngozi.<\/p>\n<ol start=\"46\">\n<li><strong>Tamaa mbele mauti nyuma: <\/strong><em>Anayetanguliza tamaa na ubinafsi huwa na mwisho mbaya.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mvulana yule alijiunga na jambazi ili kujitajirisha haraka na sasa polisi wamempiga risasi. Angejua tamaa mbele mauti nyuma.<\/p>\n<ol start=\"47\">\n<li><strong>Ukiona vinaelea, jua vimeundwa: <\/strong><em>Ukiona kitu kinakaa kizuri na kinafanya kazi yake inavyotakikana jua kwamba ni bidii na maarifa ya mtu mwingine imetoa matokeo hayo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Jana nilitembelea kiwanda cha kutengeneza gari na macho yangu yalifurahihswa kweli. Ukiona vyaelea kweli, jua vimeundwa.<\/p>\n<ol start=\"48\">\n<li><strong>Usipoziba ufa utajenga ukuta:<\/strong> <em>Usiporekebisha tatizo kama lingali changa utagharamia pakubwa baadaye.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mtoto huyu ameanza utundu. Hebu muonye mapema maana usipoziba ufa utajenga ukuta.<\/p>\n<ol start=\"49\">\n<li><strong>Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo:<\/strong> <em>Mambo yaliyopita tuachana nayo hayatudhuru, tuwaze tutavyokabiliano na yanayoukuja.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mbona unaturudisha nyuma na kuna shida kubwa zaidi yaja? Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.<\/p>\n<ol start=\"50\">\n<li><strong>Yote yang\u2019aayo si dhahabu: <\/strong><em>Usipende kitu kwa uzuri wake wa nje kwa maana si kila kitu kinachomeremeta kwa nje ni nzuri kwa ndani.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Jana nikiwa pwani nilimuona binti mrembo yuavutia sana. Karibu niende kumlaki lakini nikakumbuka babu alinionya, yote yang\u2019aayo si dhahabu.<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><strong>\u00a0<\/strong><strong>\u00a0<\/strong><\/p>\n<h3><\/h3>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Overview Methali is in bold: Meaning in italics. Examples in normal font, unformatted. &nbsp; METHALI(PROVERBS) Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo: Binadamu muungwana hutambulika na matendo yake wala si&hellip;<\/p>\n<div class=\"read-more\"><a href=\"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/kiswahili\/learn-kiswahili\/\" class=\"read-more-link\">See More<\/a><\/div>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"parent":2245,"menu_order":0,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","template":"","meta":{"jetpack_post_was_ever_published":false,"footnotes":""},"class_list":["post-2236","page","type-page","status-publish","hentry"],"jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_shortlink":"https:\/\/wp.me\/P8e7Xc-A4","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2236","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages"}],"about":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/types\/page"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2236"}],"version-history":[{"count":9,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2236\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2262,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2236\/revisions\/2262"}],"up":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2245"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2236"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}