{"id":2256,"date":"2019-11-19T17:51:26","date_gmt":"2019-11-19T17:51:26","guid":{"rendered":"http:\/\/theskrypt.co.ke\/?page_id=2256"},"modified":"2019-11-19T17:52:47","modified_gmt":"2019-11-19T17:52:47","slug":"idioms","status":"publish","type":"page","link":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/kiswahili\/idioms\/","title":{"rendered":"Idioms"},"content":{"rendered":"<h2><u>Overview<\/u><\/h2>\n<p><strong>Semi is in bold:<\/strong><\/p>\n<p><em>Meaning in italics.<\/em><\/p>\n<p>Examples in normal font, unformatted.<\/p>\n<h3><\/h3>\n<h3><strong>SEMI (IDIOMS)<\/strong><\/h3>\n<ol>\n<li><strong>Kiguu na njia<\/strong>: <em>Kutotulia mahali pamoja.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Ni vigumu sama kumpata Tanga ametulia nyumbani kwake. Yeye ni kiguu na njia.<\/p>\n<ol start=\"2\">\n<li><strong>Lila na fila<\/strong>: <em>Mema na mabaya<\/em>.<\/li>\n<\/ol>\n<p>Dunia huwa hivyo, harusi na matanga, lila na fila.<\/p>\n<ol start=\"3\">\n<li><strong>Maji kuzidi unga: <\/strong><em>Mambo kuwa mabaya au kuharibika.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Maji ilipozidi unga ilibidi auze mali yake yote ili kuishi.<\/p>\n<ol start=\"4\">\n<li><strong>Mate ya fisi:<\/strong> <em>Tamaa kubwa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Huyu mwanamume ana mate ya fisi, chochote anachokiona, anakitaka.<\/p>\n<ol start=\"5\">\n<li><strong>Mdomo na pua<\/strong>: <em>Kuwa karibu sana.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Najua anakoishi yule. Nyumbani kwangu na kwake ni mdomo na pua.<\/p>\n<ol start=\"6\">\n<li><strong>Mkono wa birika<\/strong>: <em>Kuwa mchoyo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Jirani yule hata umuombe chumvi haezi kupa. Ana mkono wa birika.<\/p>\n<ol start=\"7\">\n<li><strong>Shingo upande<\/strong>: <em>Kufanya kitu bila kupenda.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Ingawa shingo upande, ilimbidi aiage familia yake ili aende kutafuta mapato.<\/p>\n<ol start=\"8\">\n<li><strong>Uzi na sindano:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Ili kumaliza kujenga kanisa lile kwa muda wa mwezi moja, iliwabidi wanakijiji wafanye kazi kama uzi na sindano.<\/p>\n<ol start=\"9\">\n<li><strong>Kuambulia patupu:<\/strong> <em>Kukosa kabisa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Jitihada zake za kumiliki mali ya mjomba wake ziliambulia patupu ilipojulikana kwamba aliyeaga alikuwa na mrithi dhahiri.<\/p>\n<ol start=\"10\">\n<li><strong>Kuandaa meza<\/strong>:<em> Kutayarisha chakula.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mama alimuita Fatuma amusaidie kuandaa meza ili kuwapa wageni chakula.<\/p>\n<ol start=\"11\">\n<li><strong>Kuasi ukapera:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Juma alivutiwa sana na Maria na hapo akajua kwamba msichana huyo pekee ndiye atamfanya kuasi ukapera.<\/p>\n<ol start=\"12\">\n<li><strong>Kuchana mbuga: <\/strong><em>Kukimbia kutoka kwa hatari.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Wakazi walipomuona simba ameingia makaoni mwao walichana mbuga.<\/p>\n<ol start=\"13\">\n<li><strong>Kuchomea nguru:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Wenye wivu hao walimuchomea nguru kwa bosi wake na kumsababisha asipandishwe cheo kazini.<\/p>\n<ol start=\"14\">\n<li><strong>Kufa moyo:<\/strong> <em>Kupoteza matumaini.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Yule mzazi alikufa moyo baada ya mtoto wake wa kipekee kuacha shule na kuanza kutumia dawa za kulevya.<\/p>\n<ol start=\"15\">\n<li><strong>Kufua dafu:<\/strong> <em>Kufaulu\/Kushinda<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Wakimbiaji kutika Kenya walifua dafu katika michezo ya Olimpiki.<\/p>\n<ol start=\"16\">\n<li><strong>Kugonga mwamba:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Juhudi zake za kumuoa binti wa mfalme ziligonga mwamba.<\/p>\n<ol start=\"17\">\n<li><strong>Kujifunga kibwebwe: <\/strong><em>Kutia bidii.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Rono alijifunga kibwewe katika mazoezi ili aweze kusajiliwa katika mashindano ya mbio.<\/p>\n<ol start=\"18\">\n<li><strong>Kujikuna kichwa:<\/strong> <em>Kufikiria sana.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Maswali ya mtihani hio yalinifanya nikune kichwa, yalikuwa magumu sana.<\/p>\n<ol start=\"19\">\n<li><strong>Kukalia kuti kavu: <\/strong>Kutokuwa na mpango wa maisha ya baadaye.<\/li>\n<\/ol>\n<p>Amekalia kuti kavu maana pesa zote alizopokea alitumia kwa raha na sasa ana madeni.<\/p>\n<ol start=\"20\">\n<li><strong>Kukanyaga chechele: <\/strong><em>Kupotea njia.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Niliporudi kumtembelea Rehema nikiwa pekee yangu, nilikanyaga chechele.<\/p>\n<ol start=\"21\">\n<li><strong>Kukosa mbele wala nyuma<\/strong>: Kuwa maskini sana.<\/li>\n<\/ol>\n<p>Mwenye duka alimpa maskini yule mkate bila kumlipisha maana hana mbele wala nyuma.<\/p>\n<ol start=\"22\">\n<li><strong>Kukata kamba:<\/strong> <em>Kuaga dunia. <\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mgonjwa yule aliyekuwa hospitalini muda wa mwaka moja amekata kamba.<\/p>\n<ol start=\"23\">\n<li><strong>Kula kalenda<\/strong>: <em>Kufungwa jela.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Anakula kalenda baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa uhalifu aliotenda.<\/p>\n<ol start=\"24\">\n<li><strong>Kulaza damu:<\/strong> <em>Kuwa mvivu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Hakuna jambo linalo udhi kama kushiriki kazi na watu wanaopenda kulaza damu.<\/p>\n<ol start=\"25\">\n<li><strong>Kumeza mate machungu<\/strong>: <em>Kuvumilia dhiki.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Wafanyikazi wale wananyanyaswa na kazi hatari lakini wanameza mate chungu kwa sababu wanahitaji malipo.<\/p>\n<ol start=\"26\">\n<li><strong>Kuwangukia miguuni:<\/strong> <em>Kuomba msamaha.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Baada ya kuwatusi wazazi wake, aligundua makosa amefanya na kuwaangukia miguuni.<\/p>\n<ol start=\"27\">\n<li><strong>Kung\u2019oa nanga:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Meli ya kuelekea Ushelisheli iling\u2019oa nanga mwendo wa saa mbili asubuhi.<\/p>\n<ol start=\"28\">\n<li><strong>Kuona ashekari: <\/strong><em>Kupona<\/em><strong>.<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Ali ameona ashekari baada ya kuugua malaria wiki lilopita.<\/p>\n<ol start=\"29\">\n<li><strong>Kupandwa na mori:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Aliporudi nyumbani akamukosa mke wake na watoto alipandwa na mori.<\/p>\n<ol start=\"30\">\n<li><strong>Kupiga darubini:<\/strong> <em>Kufanya uchunguzi<\/em>.<\/li>\n<\/ol>\n<p>Mume yule alijipata matatani mke wake alipopiga darubini na kugundua kwamba anamutongoza mwanamke mwengine.<\/p>\n<ol start=\"31\">\n<li><strong>Kupiga dua<\/strong>: <em>Kuomba Mungu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Shida zinapozidi, wao huenda kanisani kupiga dua.<\/p>\n<ol start=\"32\">\n<li><strong>Kupiga hatua:<\/strong> <em>Kuendelea mbele<\/em>.<\/li>\n<\/ol>\n<p>Alipiga hatua mara tu alipopata mtu wakudhamini mradi wake.<\/p>\n<ol start=\"33\">\n<li><strong>Kupiga miayo:<\/strong> <em>Kupanua kinywa na kutoa pumzi kama dalili ya usingizi, njaa au kuchoka.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mwalimu alipoendelea kufunza baada ya kengele ya chakula cha mchana kupigwa, wanafunzi walianza kupiga miayo.<\/p>\n<ol start=\"34\">\n<li><strong>Kupiga moyo konde:<\/strong> <em>Kujipa nguvu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mhubiri aliwahimiza kupiga moyo konde wakati wanapokabiliwa na mateso za kidunia.<\/p>\n<ol start=\"35\">\n<li><strong>Kupigwa kalamu:<\/strong> <em>Kufutwa kazi.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Baba yake alikosa pesa za kumlipia ada katika chuo kikuu baada ya kupigwa kalamu.<\/p>\n<ol start=\"36\">\n<li><strong>Kushukiwa na nyota ya jaha:<\/strong> <em>Kuwa na bahati.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kila anapocheza mchezo wa bahati nasibu, yeye hushukiwa na nyota ya jaha maana hakosi kushinda.<\/p>\n<ol start=\"37\">\n<li><strong>Kutafuta unga:<\/strong> <em>Kufanya kazi.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kazi ni kazi, mtu hachagui, lazima kutafuta unga.<\/p>\n<ol start=\"38\">\n<li><strong>Kutoa mkono wa tanzia:<\/strong> <em>Kumpa mtu pole wakati wa msiba.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mfanyakazi mwenzetu alipofiwa na mwenziwe, tulienda kumtembelea ili kumpa mkono wa tanzia.<\/p>\n<ol start=\"39\">\n<li><strong>Kutiwa mbaroni:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Ukivunja sheria utatiwa mbaroni.<\/p>\n<ol start=\"40\">\n<li><strong>Kutoa lulu: <\/strong><em>Kuongea maneno yaliyo na busara.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Kila anapozungumza, raia wote humsikiza maana ye hutoa lulu.<\/p>\n<ol start=\"41\">\n<li><strong>Kutoa ngebe<\/strong>: <em>Kuongea maneno mengi yasiyo na maana.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mwanasiasa yule hana muhimu la kutueleza. Kazi yake ni kutoa ngebe.<\/p>\n<ol start=\"42\">\n<li><strong>Kutonesha kidonda: <\/strong><em>Kumbusha kitu kinachoumiza.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Halima hana furaha. Mpenzi wake wa sasa amerudia makosa ya mpenzi wake wa kale. Amemtonesha kidonda.<\/p>\n<ol start=\"43\">\n<li><strong>Kutumbukia kisimani:<\/strong> <em>Kuingia katika shida ambayo ni ngumu kujitoa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mtalii alipokamatwa bila pasipoti au cheti chochote cha kujitambulisha, alijua ametumbukia kisimani.<\/p>\n<ol start=\"44\">\n<li><strong>Kutupa macho<\/strong>: <em>Kuangalia mbali unapotafuta kitu.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Ndege ilipotua, alitupa macho katika umati wa watu akimtafuta mgeni wake.<\/p>\n<ol start=\"45\">\n<li><strong>Kuvalia miwani:<\/strong><\/li>\n<\/ol>\n<p>Daktari alimuonya kwamba aache kunywa pombe lakini akaivalia miwani onyo hilo.<\/p>\n<ol start=\"46\">\n<li><strong>Kuvuliwa mbeleko<\/strong>:<\/li>\n<\/ol>\n<p>Amina alivuliwa mbeleko baada ya rafikiye kutangaza mambo yake ya siri hadharani.<\/p>\n<ol start=\"47\">\n<li><strong>Kuvunja ungo<\/strong>: <em>Kukomaa kwa mtoto wa kike.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Sanasana wasichana huvunga ungo wakifikisha miaka kumi na tatu.<\/p>\n<ol start=\"48\">\n<li><strong>Kuzunguka mbuyu<\/strong>: <em>Kutoa hongo\/rushwa.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Yule polisi alimtaka dereva azunguke mbuyu ndiposa aliwachilie gari lake.<\/p>\n<ol start=\"49\">\n<li><strong>Kwenda mrama<\/strong>: <em>Kuharibikia kwa jambo au mambo.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Maisha ilipomwendea mrama, aliamua kujiua.<\/p>\n<ol start=\"50\">\n<li><strong>Kwenda msalani<\/strong>: <em>Kwenda chooni.<\/em><\/li>\n<\/ol>\n<p>Mwanafunzi aliposhindwa na mazoezi ya ziada, alimuomba mwalimu ruhusa ya kwenda msalani.<\/p>\n<p><strong>\u00a0<\/strong><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Overview Semi is in bold: Meaning in italics. Examples in normal font, unformatted. SEMI (IDIOMS) Kiguu na njia: Kutotulia mahali pamoja. Ni vigumu sama kumpata Tanga ametulia nyumbani kwake. Yeye&hellip;<\/p>\n<div class=\"read-more\"><a href=\"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/kiswahili\/idioms\/\" class=\"read-more-link\">See More<\/a><\/div>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"parent":2245,"menu_order":0,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","template":"","meta":{"jetpack_post_was_ever_published":false,"footnotes":""},"class_list":["post-2256","page","type-page","status-publish","hentry"],"jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_shortlink":"https:\/\/wp.me\/P8e7Xc-Ao","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2256","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages"}],"about":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/types\/page"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2256"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2256\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2260,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2256\/revisions\/2260"}],"up":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/2245"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/theskrypt.co.ke\/index.php\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2256"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}